Native Bible

Job 40:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

Job 40:14 in English

Job 40:14 · Berean Standard Bible

Then I will confess to you that your own right hand can save you.

Context

12mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo. 13Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini. 14Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa. 15“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,* niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe. 16Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.