Native Bible

Job 37:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.

Job 37:5 in English

Job 37:5 · Berean Standard Bible

God thunders wondrously with His voice; He does great things we cannot comprehend.

Context

3Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia. 4Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi. 5Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu. 6Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ 7Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.