Native Bible

Job 36:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu.

Job 36:3 in English

Job 36:3 · Berean Standard Bible

I get my knowledge from afar, and I will ascribe justice to my Maker.

Context

1Elihu akaendelea kusema: 2“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. 3Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu. 4Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. 5“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.