Ayubu 3:7
Job 3:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiku ule na uwe tasa; sauti ya furaha na isisikike ndani yake.
Job 3:7 in English
Job 3:7 · Berean Standard Bible
Behold, may that night be barren; may no joyful voice come into it.
Context
5Giza na kivuli kikuu kiikalie tena;
wingu na likae juu yake;
weusi na uifunike nuru yake. 6Usiku ule na ushikwe na giza kuu;
usihesabiwe katika siku za mwaka,
wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote. 7Usiku ule na uwe tasa;
sauti ya furaha na isisikike ndani yake. 8Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku,
wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.* 9Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;
nao ungojee mwanga bila mafanikio,
wala usiuone mwonzi wa kwanza
wa mapambazuko,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.