Native Bible

Job 29:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.

Job 29:12 in English

Job 29:12 · Berean Standard Bible

because I rescued the poor who cried out and the fatherless who had no helper.

Context

10wenye vyeo wakanyamazishwa, nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao. 11Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, nao walioniona walinisifu, 12kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia. 13Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba. 14Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.