Ayubu 25
Job 25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu: 2“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;
yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. 3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?
Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? 4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? 5Ikiwa hata mwezi sio mwangavu
nazo nyota si safi machoni pake, 6sembuse mtu ambaye ni funza:
mwanadamu ambaye ni buu tu!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.