Ayubu 24:15
Job 24:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ naye huuficha uso wake.
Job 24:15 in English
Job 24:15 · Berean Standard Bible
The eye of the adulterer watches for twilight. Thinking, ‘No eye will see me,’ he covers his face.
Context
13“Wako wale wanaoiasi nuru,
wasiofahamu njia zake
wala hawakai katika mapito yake. 14Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka
naye huwaua maskini na mhitaji;
wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. 15Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,
naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’
naye huuficha uso wake. 16Katika giza, huvunja majumba,
lakini wakati wa mchana hujifungia ndani;
hawataki kufanya lolote nuruni. 17Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;
hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.