Ayubu 24:13
Job 24:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake.
Job 24:13 in English
Job 24:13 · Berean Standard Bible
Then there are those who rebel against the light, not knowing its ways or staying on its paths.
Context
11Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia;
hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. 12Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini,
nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada.
Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote
kwa kutenda mabaya. 13“Wako wale wanaoiasi nuru,
wasiofahamu njia zake
wala hawakai katika mapito yake. 14Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka
naye huwaua maskini na mhitaji;
wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. 15Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,
naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’
naye huuficha uso wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.