Ayubu 16:7
Job 16:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
Job 16:7 in English
Job 16:7 · Berean Standard Bible
Surely He has now exhausted me; You have devastated all my family.
Context
5Lakini kinywa changu kingewatia moyo;
faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 6“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi;
nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. 7Ee Mungu, hakika umenichakaza;
umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote. 8Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi;
nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu. 9Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake,
na kunisagia meno yake;
adui yangu hunikazia macho yake makali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.