Ayubu 16:5
Job 16:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
Job 16:5 in English
Job 16:5 · Berean Standard Bible
But I would encourage you with my mouth, and the consolation of my lips would bring relief.
Context
3Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho?
Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 4Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi,
kama mngekuwa katika hali yangu;
ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu,
na kuwatikisia ninyi kichwa changu. 5Lakini kinywa changu kingewatia moyo;
faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 6“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi;
nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. 7Ee Mungu, hakika umenichakaza;
umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.