Native Bible

Job 16:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu.

Job 16:4 in English

Job 16:4 · Berean Standard Bible

I could also speak like you if you were in my place; I could heap up words against you and shake my head at you.

Context

2“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! 3Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 4Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu. 5Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 6“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.