Ayubu 16:11
Job 16:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.
Job 16:11 in English
Job 16:11 · Berean Standard Bible
God has delivered me to unjust men; He has thrown me to the clutches of the wicked.
Context
9Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake,
na kunisagia meno yake;
adui yangu hunikazia macho yake makali. 10Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki;
hunipiga shavuni mwangu kwa dharau,
na kuungana pamoja dhidi yangu. 11Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya,
na kunitupa katika makucha ya waovu. 12Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja;
amenikamata shingo na kuniponda.
Amenifanya mimi kuwa shabaha yake; 13wapiga upinde wake wananizunguka.
Bila huruma, huchoma figo zangu,
na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.