Ayubu 15:32
Job 15:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake, nayo matawi yake hayatastawi.
Job 15:32 in English
Job 15:32 · Berean Standard Bible
It will be paid in full before his time, and his branch will not flourish.
Context
30Hatatoka gizani;
mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,
nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali. 31Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,
kwa kuwa hatapata malipo yoyote. 32Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake,
nayo matawi yake hayatastawi. 33Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva,
kama mzeituni unaodondosha maua yake. 34Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa,
nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.