Native Bible

Job 13:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?

Job 13:11 in English

Job 13:11 · Berean Standard Bible

Would His majesty not terrify you? Would the dread of Him not fall upon you?

Context

9Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu? 10Hakika angewakemea kama mkiwapendelea watu kwa siri. 11Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi? 12Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. 13“Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.