Ayubu 11:18
Job 11:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini; utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.
Job 11:18 in English
Job 11:18 · Berean Standard Bible
You will be secure, because there is hope, and you will look around and lie down in safety.
Context
16Hakika utaisahau taabu yako,
utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita. 17Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri,
nalo giza litakuwa kama alfajiri. 18Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini;
utatazama pande zote na kupumzika kwa salama. 19Utalala, wala hakuna atakayekuogofya,
naam, wengi watajipendekeza kwako. 20Bali macho ya waovu hayataona,
wokovu utawaepuka;
tarajio lao litakuwa ni hangaiko
la mtu anayekata roho.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.