Native Bible

Job 10:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.

Job 10:14 in English

Job 10:14 · Berean Standard Bible

If I sinned, You would take note, and would not acquit me of my iniquity.

Context

12Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu. 13“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako: 14Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa. 15Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu. 16Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.