Yohana 9:26
John 9:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?”
John 9:26 in English
John 9:26 · Berean Standard Bible
“What did He do to you?” they asked. “How did He open your eyes?”
Context
24Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.” 25Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.” 26Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” 27Akawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?” 28Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake, Sisi ni wanafunzi wa Mose.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.