Native Bible

John 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakamleta kwa Mafarisayo yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali.

John 9:13 in English

John 9:13 · Berean Standard Bible

They brought to the Pharisees the man who had been blind.

Context

11Yeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu, ndipo nikanawa nami nikapata kuona!” 12Wale wakamuuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.” 13Wakamleta kwa Mafarisayo yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali. 14Basi siku hiyo Yesu alipotengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato. 15Mafarisayo nao wakaanza kumuuliza alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.