Native Bible

John 8:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti.

John 8:17 in English

John 8:17 · Berean Standard Bible

Even in your own Law it is written that the testimony of two men is valid.*

Context

15Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu, mimi simhukumu mtu yeyote. 16Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma. 17Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti. 18Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.” 19Ndipo wakamuuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?” Yesu akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hammfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.