Native Bible

John 8:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma.

John 8:16 in English

John 8:16 · Berean Standard Bible

But even if I do judge, My judgment is true, because I am not alone; I am with the Father who sent Me.*

Context

14Yesu akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli kwa sababu najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. 15Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu, mimi simhukumu mtu yeyote. 16Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma. 17Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti. 18Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.