Yohana 7:43
John 7:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu.
John 7:43 in English
John 7:43 · Berean Standard Bible
So there was division in the crowd because of Jesus.
Context
41Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!”
Lakini wengine wakauliza, “Je, Kristo kwao ni Galilaya? 42Je, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” 43Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu. 44Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa. 45Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.