Yohana 5:12
John 5:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”
John 5:12 in English
John 5:12 · Berean Standard Bible
“Who is this man who told you to pick it up and walk?” they asked.
Context
10Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.” 11Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ” 12Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?” 13Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo. 14Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.