Yohana 4:25
John 4:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
John 4:25 in English
John 4:25 · Berean Standard Bible
The woman said, “I know that Messiah” (called Christ) “is coming. When He comes, He will explain everything to us.”
Context
23Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 24Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.” 26Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.” 27Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.