Yohana 20:28
John 20:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”
John 20:28 in English
John 20:28 · Berean Standard Bible
Thomas replied, “My Lord and my God!”
Context
26Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 27Kisha akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.” 28Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.” 30Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.