Native Bible

John 20:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.

John 20:14 in English

John 20:14 · Berean Standard Bible

When she had said this, she turned around and saw Jesus standing there; but she did not recognize that it was Jesus.

Context

12naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni. 13Wakamuuliza Maria, “Mwanamke, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.” 14Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua. 15Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?” Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.” 16Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.