Yohana 20:16
John 20:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).
John 20:16 in English
John 20:16 · Berean Standard Bible
Jesus said to her, “Mary.” She turned and said to Him in Hebrew,* “Rabboni!” (which means “Teacher”).
Context
14Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua. 15Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?”
Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.” 16Yesu akamwita, “Maria!”
Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu). 17Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ” 18Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, “Nimemwona Bwana!” Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.