Native Bible

John 12:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.”

John 12:32 in English

John 12:32 · Berean Standard Bible

And I, when I am lifted up from the earth, will draw everyone to Myself.”

Context

30Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 31Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33Yesu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa. 34Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Sheria kwamba ‘Kristo* adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.