Yohana 12:31
John 12:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
John 12:31 in English
John 12:31 · Berean Standard Bible
Now judgment is upon this world; now the prince of this world will be cast out.
Context
29Ule umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.” 30Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 31Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33Yesu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.