Native Bible

John 11:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”

John 11:40 in English

John 11:40 · Berean Standard Bible

Jesus replied, “Did I not tell you that if you believed, you would see the glory of God?”

Context

38Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake. 39Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.” Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.” 40Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” 41Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Yesu akainua macho yake juu akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. 42Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.