Yohana 11:38
John 11:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake.
John 11:38 in English
John 11:38 · Berean Standard Bible
Jesus, once again deeply moved, came to the tomb. It was a cave with a stone laid across the entrance.
Context
36Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!” 37Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?” 38Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake. 39Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.”
Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.” 40Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.