Native Bible

John 11:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu.

John 11:29 in English

John 11:29 · Berean Standard Bible

And when Mary heard this, she got up quickly and went to Him.

Context

27Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo,* Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.” 28Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.” 29Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu. 30Yesu alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. 31Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.