Yohana 1:20
John 1:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”*
John 1:20 in English
John 1:20 · Berean Standard Bible
He did not refuse to confess, but openly declared, “I am not the Christ.”
Context
18Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha. 19Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”* 21Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”
Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”
“Je, wewe ni yule Nabii?”
Akajibu, “Hapana.” 22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.