Yeremia 9:10
Jeremiah 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo, milio ya ngʼombe haisikiki. Ndege wa angani wametoroka na wanyama wamekimbia.
Jeremiah 9:10 in English
Jeremiah 9:10 · Berean Standard Bible
I will take up a weeping and wailing for the mountains, a dirge over the wilderness pasture, for they have been scorched so no one passes through, and the lowing of cattle is not heard. Both the birds of the air and the beasts have fled; they have gone away.
Context
8Ndimi zao ni mshale wenye sumu,
hunena kwa udanganyifu.
Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,
lakini moyoni mwake humtegea mtego. 9Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”
asema Bwana.
“Je, nisijilipizie kisasi
kwa taifa kama hili?” 10Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima
na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.
Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,
milio ya ngʼombe haisikiki.
Ndege wa angani wametoroka
na wanyama wamekimbia. 11“Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,
makao ya mbweha;
nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa
ili asiwepo atakayeishi humo.” 12Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.