Yeremia 8:18
Jeremiah 8:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Mfariji wangu katika huzuni, moyo wangu umezimia ndani yangu.
Jeremiah 8:18 in English
Jeremiah 8:18 · Berean Standard Bible
My sorrow is beyond healing;* my heart is faint within me.
Context
16Mkoromo wa farasi za adui
umesikika kuanzia Dani,
kwa mlio wa madume yao ya farasi,
nchi yote inatetemeka.
Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo,
mji na wote waishio ndani yake.” 17“Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali katikati yenu,
fira ambao hawawezi kulogwa,
nao watawauma,”
asema Bwana. 18Ee Mfariji wangu katika huzuni,
moyo wangu umezimia ndani yangu. 19Sikia kilio cha watu wangu
kutoka nchi ya mbali:
“Je, Bwana hayuko Sayuni?
Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”
“Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,
kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?” 20“Mavuno yamepita,
kiangazi kimekwisha,
nasi hatujaokolewa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.