Yeremia 52:29
Jeremiah 52:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza, watu 832 kutoka Yerusalemu;
Jeremiah 52:29 in English
Jeremiah 52:29 · Berean Standard Bible
in Nebuchadnezzar’s eighteenth year, 832 people from Jerusalem;
Context
27Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe.
Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao. 28Hii ndiyo hesabu ya watu ambao Nebukadneza aliwachukua kwenda uhamishoni:
katika mwaka wa saba,
Wayahudi 3,023; 29katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza,
watu 832 kutoka Yerusalemu; 30katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake,
Wayahudi 745 walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme.
Jumla ya watu wote walikuwa 4,600. 31Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki* alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini mfalme wa Yuda, na kumfungua kutoka gerezani siku ya ishirini na tano ya mwezi wa kumi na mbili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.