Yeremia 52:27
Jeremiah 52:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao.
Jeremiah 52:27 in English
Jeremiah 52:27 · Berean Standard Bible
There at Riblah in the land of Hamath, the king of Babylon struck them down and put them to death. So Judah was taken into exile, away from its own land.
Context
25Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri saba wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji. 26Nebuzaradani jemadari akawachukua hao wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. 27Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe.
Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao. 28Hii ndiyo hesabu ya watu ambao Nebukadneza aliwachukua kwenda uhamishoni:
katika mwaka wa saba,
Wayahudi 3,023; 29katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza,
watu 832 kutoka Yerusalemu;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.