Native Bible

Jeremiah 50:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! Watakuwa wapumbavu. Upanga dhidi ya mashujaa wake! Watajazwa na hofu kuu

Jeremiah 50:36 in English

Jeremiah 50:36 · Berean Standard Bible

A sword is against her false prophets, and they will become fools. A sword is against her warriors, and they will be filled with terror.

Context

34Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli. 35“Upanga dhidi ya Wakaldayo!” asema Bwana, “dhidi ya wale waishio Babeli na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara! 36Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! Watakuwa wapumbavu. Upanga dhidi ya mashujaa wake! Watajazwa na hofu kuu 37Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! Wao watakuwa kama wanawake. Upanga dhidi ya hazina zake! Hizo zitatekwa nyara. 38Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.