Native Bible

Jeremiah 50:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Jeremiah 50:25 in English

Jeremiah 50:25 · Berean Standard Bible

The LORD has opened His armory and brought out His weapons of wrath, for this is the work of the Lord GOD of Hosts in the land of the Chaldeans.

Context

23Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa! 24Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Bwana. 25Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo. 26Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote. 27Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.