Yeremia 50:27
Jeremiah 50:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.
Jeremiah 50:27 in English
Jeremiah 50:27 · Berean Standard Bible
Kill all her young bulls; let them go down to the slaughter. Woe to them, for their day has come— the time of their punishment.
Context
25Bwana amefungua ghala lake la silaha
na kuzitoa silaha za ghadhabu yake,
kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote
anayo kazi ya kufanya
katika nchi ya Wakaldayo. 26Njooni dhidi yake kutoka mbali.
Zifungueni ghala zake za nafaka;
mlundikeni kama lundo la nafaka.
Mwangamizeni kabisa
na msimwachie mabaki yoyote. 27Waueni mafahali wake wachanga wote;
waacheni washuke machinjoni!
Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia,
wakati wao wa kuadhibiwa. 28Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli
wakitangaza katika Sayuni
jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi,
kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. 29“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli,
wote wale wavutao upinde.
Pigeni kambi kumzunguka kabisa,
asitoroke mtu yeyote.
Mlipizeni kwa matendo yake;
mtendeeni kama alivyotenda.
Kwa kuwa alimdharau Bwana,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.