Yeremia 50:22
Jeremiah 50:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu!
Jeremiah 50:22 in English
Jeremiah 50:22 · Berean Standard Bible
“The noise of battle is in the land— the noise of great destruction.
Context
20Katika siku hizo, wakati huo,”
asema Bwana,
“uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli,
lakini halitakuwepo,
kwa ajili ya dhambi za Yuda,
lakini haitapatikana hata moja,
kwa kuwa nitawasamehe
mabaki nitakaowaacha. 21“Shambulieni nchi ya Merathaimu
na wale waishio huko Pekodi.
Wafuatieni, waueni
na kuwaangamiza kabisa,”
asema Bwana.
“Fanyeni kila kitu nilichowaamuru. 22Kelele ya vita iko ndani ya nchi,
kelele ya maangamizi makuu! 23Tazama jinsi nyundo ya dunia yote
ilivyovunjika na kuharibika!
Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa
miongoni mwa mataifa! 24Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli,
nawe ukakamatwa kabla haujafahamu;
ulipatikana na ukakamatwa
kwa sababu ulimpinga Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.