Native Bible

Jeremiah 50:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Jeremiah 50:21 in English

Jeremiah 50:21 · Berean Standard Bible

Go up against the land of Merathaim, and against the residents of Pekod. Kill them * and devote them to destruction.* Do all that I have commanded you,” declares the LORD.

Context

19Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe naye atalisha huko Karmeli na Bashani; njaa yake itashibishwa juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi. 20Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha. 21“Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru. 22Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu! 23Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.