Yeremia 5:20
Jeremiah 5:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Itangazie nyumba ya Yakobo hili na ulipigie mbiu katika Yuda:
Jeremiah 5:20 in English
Jeremiah 5:20 · Berean Standard Bible
Declare this in the house of Jacob and proclaim it in Judah:
Context
18“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana. 19“Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’ 20“Itangazie nyumba ya Yakobo hili
na ulipigie mbiu katika Yuda: 21Sikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili,
mlio na macho lakini hamwoni,
mlio na masikio lakini hamsikii: 22Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Bwana.
“Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?
Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,
kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.
Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;
yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.