Yeremia 49:6
Jeremiah 49:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini hatimaye, nitarudisha mateka wa Waamoni,” asema Bwana.
Jeremiah 49:6 in English
Jeremiah 49:6 · Berean Standard Bible
Yet afterward I will restore the Ammonites from captivity,*” declares the LORD.
Context
4Kwa nini unajivunia mabonde yako,
kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana?
Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema,
‘Ni nani atakayenishambulia?’ 5Nitaleta hofu kuu juu yako
kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.
“Kila mmoja wenu ataondolewa,
wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi. 6“Lakini hatimaye,
nitarudisha mateka wa Waamoni,”
asema Bwana. 7Kuhusu Edomu:
Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Je, hakuna tena hekima katika Temani?
Je, shauri limewapotea wenye busara?
Je, hekima yao imechakaa? 8Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,
wewe uishiye Dedani,
kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau
wakati nitakapomwadhibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.