Yeremia 49:21
Jeremiah 49:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka. Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.*
Jeremiah 49:21 in English
Jeremiah 49:21 · Berean Standard Bible
At the sound of their fall the earth will quake; their cry will resound to the Red Sea.*
Context
19“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani
kuja kwenye nchi ya malisho mengi,
ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.
Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?
Ni nani aliye kama mimi,
na ni nani awezaye kunipinga?
Tena ni mchungaji yupi awezaye
kusimama kinyume nami?” 20Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Edomu,
kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:
Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;
yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. 21Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.
Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.* 22Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,
akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.
Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu
itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 23Kuhusu Dameski:
“Hamathi na Arpadi imetahayarika,
kwa kuwa wamesikia habari mbaya.
Wamevunjika moyo na wametaabika
kama bahari iliyochafuka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.