Yeremia 49:17
Jeremiah 49:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya; wote wapitao karibu watashangaa na kuzomea kwa sababu ya majeraha yake yote.
Jeremiah 49:17 in English
Jeremiah 49:17 · Berean Standard Bible
“Edom will become an object of horror. All who pass by will be appalled and will scoff at all her wounds.
Context
15“Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,
aliyedharauliwa miongoni mwa watu. 16Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako
vimekudanganya,
wewe unayeishi katika majabali ya miamba,
wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.
Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,
nitakushusha chini kutoka huko,”
asema Bwana. 17“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;
wote wapitao karibu
watashangaa na kuzomea
kwa sababu ya majeraha yake yote. 18Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,
pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”
asema Bwana,
“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.
Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo. 19“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani
kuja kwenye nchi ya malisho mengi,
ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.
Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?
Ni nani aliye kama mimi,
na ni nani awezaye kunipinga?
Tena ni mchungaji yupi awezaye
kusimama kinyume nami?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.