Yeremia 48:26
Jeremiah 48:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mlevye, kwa kuwa amemdharau Bwana. Moabu na agaegae katika matapishi yake, yeye na awe kitu cha dhihaka.
Jeremiah 48:26 in English
Jeremiah 48:26 · Berean Standard Bible
“Make him drunk, because he has magnified himself against the LORD; so Moab will wallow in his own vomit, and he will also become a laughingstock.
Context
24katika Keriothi na Bosra;
kwa miji yote ya Moabu,
iliyoko mbali na karibu. 25Pembe* ya Moabu imekatwa,
mkono wake umevunjwa,”
asema Bwana. 26“Mlevye,
kwa kuwa amemdharau Bwana.
Moabu na agaegae katika matapishi yake,
yeye na awe kitu cha dhihaka. 27Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?
Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,
kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau
kila mara unapozungumza juu yake? 28Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,
enyi mnaoishi Moabu.
Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake
kwenye mdomo wa pango.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.