Yeremia 48:15
Jeremiah 48:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
Jeremiah 48:15 in English
Jeremiah 48:15 · Berean Standard Bible
Moab has been destroyed and its towns have been invaded; the best of its young men have gone down in the slaughter, declares the King, whose name is the LORD of Hosts.
Context
13Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,
kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu
walipotegemea mungu wa Betheli.* 14“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,
watu jasiri katika vita’? 15Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,
vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”
asema Mfalme, ambaye jina lake
ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. 16“Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,
janga kubwa litamjia kwa haraka. 17Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,
ninyi nyote mnaojua sifa zake,
semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,
tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.