Yeremia 48:13
Jeremiah 48:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu walipotegemea mungu wa Betheli.*
Jeremiah 48:13 in English
Jeremiah 48:13 · Berean Standard Bible
Then Moab will be ashamed of Chemosh, just as the house of Israel was ashamed when they trusted in Bethel.
Context
11“Moabu amestarehe tangu ujana wake,
kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,
haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,
hajaenda uhamishoni.
Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,
nayo harufu yake haijabadilika. 12Lakini siku zinakuja,”
asema Bwana,
“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,
nao watamimina;
wataacha magudulia yake yakiwa matupu
na kuvunja mitungi yake. 13Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,
kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu
walipotegemea mungu wa Betheli.* 14“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,
watu jasiri katika vita’? 15Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,
vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”
asema Mfalme, ambaye jina lake
ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.