Yeremia 48:11
Jeremiah 48:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika.
Jeremiah 48:11 in English
Jeremiah 48:11 · Berean Standard Bible
Moab has been at ease from youth, settled like wine on its dregs; he has not been poured from vessel to vessel or gone into exile. So his flavor has remained the same, and his aroma is unchanged.
Context
9Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,
kwa kuwa ataangamizwa;
miji yake itakuwa ukiwa,
pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake. 10“Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila!
Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu! 11“Moabu amestarehe tangu ujana wake,
kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,
haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,
hajaenda uhamishoni.
Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,
nayo harufu yake haijabadilika. 12Lakini siku zinakuja,”
asema Bwana,
“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,
nao watamimina;
wataacha magudulia yake yakiwa matupu
na kuvunja mitungi yake. 13Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,
kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu
walipotegemea mungu wa Betheli.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.