Yeremia 48:17
Jeremiah 48:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, ninyi nyote mnaojua sifa zake, semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu, tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’
Jeremiah 48:17 in English
Jeremiah 48:17 · Berean Standard Bible
Mourn for him, all you who surround him, everyone who knows his name; tell how the mighty scepter is shattered— the glorious staff!
Context
15Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,
vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”
asema Mfalme, ambaye jina lake
ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. 16“Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,
janga kubwa litamjia kwa haraka. 17Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,
ninyi nyote mnaojua sifa zake,
semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,
tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’ 18“Shuka kutoka fahari yako
na uketi katika ardhi iliyokauka,
enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,
kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako,
na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma. 19Simama kando ya barabara na utazame,
wewe unayeishi Aroeri.
Muulize mwanaume anayekimbia
na mwanamke anayetoroka,
waulize, ‘Kumetokea nini?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.